Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

YANGA YAENDELEZA UTEJA KWA SIMBA SC


Na Samuel Samuel

Mchezo wa kirafiki baina ya Simba na Yanga maarufu kama "Mtani Jembe" umemalizika leo katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam huku Simba wakiondoka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Awadhi Juma na Elius Maguli kipindi cha kwanza.
 
Simba SC ikiwatumia wachezaji wake mahiri kama Emmanuel Okwi, Maguli, Sserunkuma, Awadhi na mkongwe Ivo Mapunda wameendeleza ubabe wao kwa vijana wa Jangwani. 

Yanga wasitafute mchawi bali wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuipenya ngome ya Simba dk 15 za mwanzo ambazo Simba walionesha kutoelewana. 

Lakini baada ya Simba SC kujua makosa yao na Simon Sserunkuma, Okwi na Maguli kuelewana vizuri basi ndo mabeki wa Yanga walipoanza kuhenyeshwa na kasi ya mashambulizi hayo. 

 Kiufupi mabeki wa kati wa Yanga Nadir na Yondani walishindwa kabisa kuimudu kasi hiyo. Simba imebebwa vizuri sana na Okwi leo aliyeichachafya vilivyo beki ya Yanga. 

Maximo kama angeliwanzisha mapema Danny Mrwanda na Salum Telela basi matokeo yangebadilika. Kutoka kwa Coutinho , Twite na Sherman kuliipa uhai Yanga.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!