Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Gervinho aichukia Arsenal


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya AS Roma ya Italia, Gervinho aelezea jinsi gani anavyoichukia Arsenal huku chanzo kikiwa ni kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger.

Gervinho alyekipiga kwenye timu hiyo yenye maskani yake jijini London kwa miaka miwili toka 2011-2013 akisajiliwa kutokea timu ya Lille ya nchini Ufaransa kwa ada ya karibu pauni milioni 10.8.

Lakini katika kipindi chote Gervinho alishindwa kuwika na hatimaye kuuzwa kwa timu ya Roma mwezi wa nane 2013.

Akiongea na gazeti la Gazzetta dello Sport la nchini Italia Gervinho alisema “Wenger hakuwahi kuwa na imani na mimi, nikiwa mtoto niliota kuichezea Arsenal kwasababu nliwapenda kwasasa nawachukia kwa jinsi Wenger alivyonitendea”

“Ingawa najutia kuondoka baada ya muda mfupi bila kuonyesha thamani yangu ambayo kwasasa badala yake naionyesha Roma”

Gervinho mwenye umri wa miaka 27 aliichezea Arsenal michezo 46 huku akiifungia magoli tisa tu kabla ya kuuzwa kuichezea timu ya AS Roma kitendo ambacho binafsi Gervinho hakukifurahia ingawa kwasasa amekuwa nyota wa kutegemewa kwenye timu hiyo kwenye ligi ya nchini Italia maarufu kama SERIE A.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!