Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Anaipenda Yanga, Yanga haimpendi!Samuel Samuel

Omega Seme amekuwa hana Bahati na klabu anayoipenda sana (Yanga). Si Maximo tu ambaye amemnyina fursa ya kuitumikia KLABU hiyo bali toka uwepo wa kocha Ernie Brandts ulimkataa kiungo huyo. Msimu wa 2013-14 Brandts alimpeleka Tanzania Prison kwa mkopo. 

Na hiyo ilitokana na Yanga kusheheni wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi hiyo ya kiungo chini. Wachezaji hao ni Athuman Chuji, Domayo, Salum Telela na Bakari Masoud. 

Kuondoka kwa Chuji, Bakari, Domayo kulimrudisha Omega Jangwani baada ya Maximo kuamua kumtumia Salum Telela kama beki wa kulia na Mbuyu Twite kupanda kama chief engineer pale kati basi Seme akaonekana kama back up kubwa kwa Twite. 

 Wahenga wanasema lakuvunda halina ubani. Mara zote Maximo alipompa nafasi dogo alionesha yupo flat, ana kaa sana na mpira na uwezo mdogo kupandisha timu. 

Hivyo Yanga ikahitaji suluhisho na Mbrazil Emerson akatokea hivyo kufungua mlango kwa Seme kuondoka. Seme ametua Ndanda FC

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!