Wachezaji wa Bongo na maisha ya Clouds Fm.
Na Mwandishi wetu
Achana na muziki wa bolingo, achana na muziki wa taarabu, mziki wa bongo flava ndio unavuma kwa sasa hapa nchini kwetu. Sifa kuu ya muziki hu ni kupata umaarufu, mtaani tunaita "kick" ikimaanisha sifa na umaarufu tu akuna zaidi.
Wapo wasanii wachache kidogo wanaupeleka mbele muziki huu kwenye levo za kimataifa. Watu kama kina AY, wanafanya vizuri kuutangaza mziki wetu nje ya tanzania.
Wapo kina DIAMOND huyu naye kafanya poa sana. Kafanya kidogo Tanzania ijulikane nje kimuziki ila wengine tena kwa idadi kubwa, wanalewa sifa wakisikika kwenye redio basi ndio wamemaliza.
Wataanza kujisikia na kujiona wao ndio wao, wataanza kujiita masuper star huku njaa zimewajaa mfukoni. Wanaishi maisha ya kuigiza ndio U BONGO FLEVA HULIVYO sasa huu U BONGO FLEVA umeamia kwenye mpira wetu wa Tanzania.
Wachezaji wetu wamekuwa wazito kujitanua kimataifa sijui kwanini. Wakifika timu za simba, yanga au Azam wanaridhika kabisa. hizi klabu ndio kama clouds fm, time fm, etv radio,tbc fm zao yani kama wasanii vile, nyimbo zao zikichezwa hapo wamemaliza kabisa.
Japo tunao wakina DIAMOND NA AY wa soka wachache waliojitambua kujipeleka kimataifa kama Mbwana Sammata, Thomas Ulimwengu, Mwinyi kazimoto na wengine hawa wamejitambua wameonyesha waneweza.
Hivi kweli tumeshindwa kuzalisha wachezaji wengi wazuri wenye sifa za kucheza nje ya Tanzania? tuuache huu ubongo fleva kwenye soka.
kwenye bongo fleva tunaona wengi wanaenda nje kupiga shoo tu. Tunasikia Show zenyewe ni za bei chee, zile za sebuleni na kuambulia nauli ya kwenda na kurudi!
Kwenye soka nako zipo show za bei chee. Shomary Kapombe alienda kwenye show na sasa, karudi kuuendeleza u bongo fleva wake.
Majuzi tu nikasikia habari za mkude mara kaenda Azam, mara Yanga mara Simba wakamzuia. Mkude naye anaichukulia klabu ya Simba kama ndio clouds fm yake.
Hana mawazo ya kufikiria kuhusu chanel 0, Trace tv wala Mtv. Mawazo yake yameganda ki-Bongo Flava. Hata Simoni Msuva naye ana endelea kuishi ki-Bongo Flava.
Hivi vituo vya Redio na Tv za Nyumbani, havina ubaya wowote. Wanajitahidi kukuza muziki wetu lakini ni lazima mwanamuziki awe anajua kujiongeza na kufika mbele zaidi. Hizi timu za Simba na Yanga, hazina tofauti na vyombo vya habari nilivyovitaja. Wachezaji wanapaswa kujiongeza ili kufika mbali zaidi.
LINI UTAISHA HUU U-BONGO WA SOKA? NI HAYO TU -0765178880
0 comments:
Post a Comment