Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Real Madrid ni mwendo wa rekodi tu.


 Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kumpiga Ludogorets. bao 4-0 hapo jana, Real Madrid waliweza kuweka rekodi mpa kwenye soka la Hispani baada ya kushinda mechi 19 mfululizo.

Hapo awali rekodi ya kushinda mechi nyingi mfululizo ilikuwa inashikiliwa na klabu ya Barcelona ambao waliweza kucheza mechi 18 msimu wa 2005/2006 bila kupoteza.

Christiano Ronaldo alifunga bao lake la 72 kwenye klabu bingwa Ulaya na kumpita mkongwe na timu hiyo, Raul Gonzalez ambaye walikuwa wamefungana kwa kufunga mabao 71.

Gareth Bale naye akifunga kwa kichwa kabla ya Alvaro Arbeloa na kijana wa kocha Carlo Ancelotti, Alvaro Medrankutokea benchi na kufunga bao la nne.

Real Madrid wamefuzu kama vinara wa kundi B baada ya kushinda mechi zao zote sita na kujikusanyia alama 18. Fc Basel baada ya kutoka sare ya 1-1 na Liverpool, nao wanafuzu kwa hatua ya 16 bora. 

Liverpool wanakwenda Europa League baada ya kushika nafasi ya tatu huku Ludogorets wao wakimaliza kwa kushika mkia. Draw ya hatua ya 16 bora inatarajiwa kupangwa siku ya Jumatatu ambapo moja kati ya timu ambazo Real Madrid wanaweza kukutananazo ni Barcelona na Arsenal.

1 comments:

 
Back to top!