Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 December 2014
Wednesday, December 10, 2014

Kibarua cha Pellegrini kipo Salama.


 Na Oscar Oscar Jr

 Na Oscar Oscar Jr

Mshambuliaji wa Manchester City, Eden Dzeko leo anatarajia kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha kocha wa timu hiyo, Manuel Pellegrini dhidi ya As Roma mchezo utakaopigwa pale Stadio Olimpico huku timu hiyo ya Uingereza ikihitaji matokeo ya ushindi na kuombea Bayern Munich waifunge timu ya CSKA Moscow.

Dzeko ambaye bado hajapona sawasawa atalazimika kuingia dimbani na kuziba pengo lililoachwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Sergio Kun Aguero ambaye aliumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya timu ya Everton.

Mshambuliaji huyo ambaye amefunga magoli 19 kwenye mechi 21 msimu huu, anasadikika kuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki nne mpaka sita. 

Akizungumza kuelekea mpambano huo, kocha wa Manchester City amesema kuwa kibarua chake kiko salama bila kujali matokeo ya mchezo huo wa klabu bingwa Ulaya. 

Dzeko anaaminika kuwa mtu wa muhimu sana kwenye mchezo wa leo ambapo hata msimu uliopita wakati Aguero alipokuwa nje, Dzeko alichukuwa nafasi yake na kufunga magoli tisa kwenye mechi 11 za mwisho na kuisaidia City kuweza kutwaa taji la ligi kuu.

Kuelekea mchezo huo Dzeko amehojiwa na kujibu kuwa, anafuraha kurejea kwani hakuwahi kuwa nje kwa majeruhi ya muda mrefu na kilichomtokea msimu huu kidogo kilimuweka kwenye wakati mgumu na kuahidi kuwa, siku zote timu inapomuhitaji yupo kuhakikisha anatoa mchango na kufanya washinde.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!