Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Arsenal sasa watolea macho Draw ya Jumatatu.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa timu ya Stoke City, vijana wa Arsenal jana walikuwa kwenye ubora wao kwenye mechi za kumalizia makundi ya klabu bingwa Ulaya amabapo timu hiyo ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 4-1 ugenini walipocheza na Galatasaray.

Lukas Podolski ambaye amekuwa hapewi nafasi kwenye kikosi cha kwanza, jana alianza na kufunga magoli mawili huku mchezaji bora wa Arsenal wa msimu uliopita, Aaron Ramsey jana alikuwa kwenye ubora wake na kufunga naye magoli mawili huku Mdachi, Wesley Sneijder akifunga bao pekee kwa upande wa Galatasaray.

Arsenal na Borussia Dortmund wote wanaalama 13 lakini tofauti ya magoli, imewapa Borussia Dortmund nafasi ya kuongoza kundi. Arsenal wakiwa kwenye nafasi ya pili kuna uwezekano mkubwa wakapangwa na vigogo.

Timu ambazo Arsenal anaweza kukutana nazo kwenye hatua ya 16 bora ni pamoja na Real Madrid, Atletico Madrid, PSG, Bayern Munich, Monaco na Porto kutoka nchini Ureno.

Mashabiki wa Arsenal watakuwa na furaha baada ya kuona timu yao ikimaliza makundi na kutinga hatua ya mtoano na hofu pekee itakuwa siku ya Jumatatu ambapo makundi hayo yatapangwa.






0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!