Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Mke wa Falcao amwijia juu Kocha wa Manchester United




Na Florence George

Mara baada ya kuwa hapati namba ya kuanza mara kwa mara katika kikosi cha Manchester United mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao, sasa mke wa mchezaji huyo Lorelei Taron amemwijia juu kocha wa timu hiyo Luis Van Gaal akihoji kwa nini mume wake hapangwi katika kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Taron alisema kuwa anashangaa kuwa kwanini Van Gaal amekuwa  akimuweka benchi Falcao wakati mchezaji huyo yupo fiti asilimia 100 kuichezea klabu hiyo,hayo yamekuja mara baada ya Van Gaal kusema kuwa Flcao anaweza kucheza dakika 45,60 au hata 90 katika timu ya pili lakini hapendi kumpeleka huko huku akiwa anamuhijati katika benchi ili anapokosekana James Wilson au Wayne Rooney achukue nafasi zao.

Van Gaal anasema kuwa kwa sasa Falcao anauwezo wa kucheza dakika 20 katika timu ya kwanza kutokana na ligi kuu iliyo kwa sasa huku akisema kuwa hajali kama mchezaji huyo kutokuwa na furaha kukaa benchi na kusema kuwa anatakiwa kufuata Falsafa yake.

Falcao alijiunga na United kwa mkopo mwezi september mwaka huu akitokea Monaco ya nchini Ufaransa ambapo amekuwa katika kiwango cha chini huku majeruhi yakimuandama hali iliyopelekea kufunga goli moja tu hadi sasa katika ligi kuu nchini Uingereza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!