Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Kompany ,Silva kuwavaa AS Roma






Na Florence George

Klabu ya soka ya Manchester City imepata matumaini mara baada ya wachezaji wake muhimu wakiwamo nahodha wa timu hiyo Vicent Kompany pamoja na David Silva kuonekana wanaweza kucheza mchezo dhidi ya As Roma ya nchini Italia katika mchezo wa mwisho wa ligi ya mabingwa barani ulaya siku ya jumatano huko Stadio Olimpico.

Wachezaji kama Kompany ,Silva pamoja na Jovetic na Fernandinho ambao walikosekana katika mechi dhidi ya Everton jumamosi wanategemewa kuongeza nguvu katika kikosi cha City siku hiyo ya jumatano.

Kompany ambae alikosekana katika michezo miwili ya City anatazamiwa kuwapo katika mchezo huo baada ya kupona majeraha yake,huku David Silva ambae alikuwa nje ya uwanja tangu mwenzi October mara baada ya kuumia katika mechi ya Capital One dhidi ya Newcastle United.

Silva alitazamiwa kucheza katika mechi dhidi ya Everton siku ya jumamosi lakini kocha wa City Manuel Pellegrini hakumpanga akihofia kujitonesha, hivyo kwenye mchezo huo anatazamiwa kuwemo.Jovetic na Fernandinho hawakucheza mchezo dhidi ya Everton lakini sasa wapo fiti kuwavaa waitaliano hao huku Edin Dzeko aliingia kipindi cha pili mara baada ya kupona majeruhi yake.

City itamkosa mshambuliaji wake namba moja Sergio Aguero aliyeumia katika mechi dhidi ya Everton,pia itamkosa kiungo wake mahili Yaya Toure anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.

katika mchezo huo Manchester City inahijaji ushindi ili iweze kufuzu hatua ya 16 bora mara baada ya kufikisha pointi tano sawa na As Roma pamoja na CSKA Moscow huku ikiiombea Bayern Munich ishinde dhidi ya CSKA Moscow.   

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!