Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Platini amfukuza Blatter FIFA.




Na Chikoti Cico



Raisi wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michel Platini akataa kumuunga mkono Raisi wa sasa wa shirikisho la soka Duniani (FIFA) Sepp Blatter kwenye uchaguzi wa mwakani katika kuchagua Raisi mpya wa shirikisho hilo la kabumbu duniani.

Blatter aliyechaguliwa mwaka 1998 anatarajia kugombea tena kwa kipindi cha tano kuongoza tena shirikisho hilo ambalo hivi karibuni limekumbwa na kashfa ya rushwa kwenye mchakato wa kuchagua nchi mwenyeji wa fainali za kombe la Dunia kwa mwaka 2018 na 2022 nchini Urusi na Qatar kwa pamoja.

Akiongea na kituo cha redio cha Europe 1 nchini Ufaransa Platini alisema “nilimuunga mkono mwaka 1998 kwasababu nilifikiri alikuwa mtu sahihi kwa wakati ule lakini baada ya kipindi cha miaka mitano ni muda wa kuacha hali ya hewa mpya iingie na kuachia nafasi kwa mtu mwingine” aliendelea kwa kusema “Taswira ya FIFA ni mbaya sana ndiyo maana nafikiria kwamba itakuwa vyema akiacha lakini sifikiri kama anataka”.

Alipoulizwa ni nani atamuunga mkono kwenye uchaguzi huo wa Raisi mpya wa FIFA hapo mwakani kati ya Blatter na Jerome Champagne ambao wametangaza kuwania kiti hicho, Platini alisema “ hakuna, natumai wengine watagombania” .

Huku akiwa na matumaini kwa mgombea atakayetoka bara lingine zaidi ya Ulaya kushinda kama akigombania Platini aliongezea kwa kusema “mgombea mwingine toka Ulaya atakuwa na nafasi ndogo ya kushinda.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!