Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2014
Saturday, November 15, 2014

Hakuna anayepinga ubora wa mchezaji huyu


Na Chikoti Cico


Huku mchakato wa mbio za kuwania tuzo ya mchezaji bora duniani maarufu kama “Ballon d'Or winner” zikiendelea nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mshambulliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ameendelea kung’aa baada ya kuweka rekodi mpya kwenye michuano ya Ulaya (European Championship) baada ya kufikisha magoli 23, rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mshambuliaji kutoka Denmark Jon Dahl Tomasson.

Tomasson ambaye alistaafu soka mwaka 2010 aliweka rekodi hiyo kwa kufunga magoli 22 katika mechi 31 akiichezea timu ya taifa ya Denmark huku Ronaldo akivunja rekodi hiyo baada ya kufunga goli la ushindi kwenye mechi ya kufuzu michuano ya EURO 2016 dhidi ya Armenia mechi iliyoisha kwa Ureno kushinda kwa goli 1-0 na kusogea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi I huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Denmark.

Ronaldo ambaye ameanza msimu huu kwa kasi mpaka sasa amefunga magoli 23 katika mechi 17 alizoichezea Real Madrid huku kati ya magoli hayo 18 akiwa ameyafunga kwenye ligi kuu nchini Hispania maarufu kama la liga hivyo kuisadia Madrid kuongoza ligi hiyo ikiwa juu ya Barcelona kwa alama mbili baada ya michezo 11.

Kuwekwa kwa rekodi hiyo na Ronaldo kumekuja sambamba na kushinda tuzo ya mfungaji bora wa msimu uliopita kwenye la liga ambapo alifunga jumla ya magoli 31, Ronaldo ameweka rekodi hiyo mpya ya magoli 23 kwenye michuano ya Ulaya baada ya michezo 37 ya timu ya taifa ya Ureno.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!