Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Louis Van Gaal ameanza "Mchecheto wa EPL"


Na Chikoti Cico

Kocha wa Manchester United, Mdachi Luis Van Gaal alalamikia ratiba ya ligi kuu nchini Uingereza kipindi cha Desemba. Ratiba hiyo ambayo inazilazimu timu kucheza mechi tisa ndani ya siku 36, inampa wasiwasi kocha huyo ambaye mpaka sasa timu yake imecheza mechi 13 kwenye ligi hiyo toka alipochaguliwa kuifundisha United miezi minne iliyopita.

Van Gaal alimeiongoza United kushinda mchezo uliopita dhidi ya Hull City na kushika nafasi ya nne huku wakiwa na alama 22, akiongea na vyombo vya habari alisema “Sifurahii lakini siwezi kubadili, sikubaliani na hili (ratiba) kwasababu sifikiri ni vizuri kwa wachezaji wacheze mechi nyingine ndani ya siku mbili”

Aliendelea kusema “Desemba itakuwa kama hivyo, pia tuna familia, mimi pia nina mke, watoto, wajukuu na sitawaona Krismasi hii lakini nataka kufanya kazi kwenye “primia” ligi.

Natakiwa kuendana na mazingira lakini sifikiri kama ni vizuri kwa wachezaji ama kwa familia” Baada ya mechi dhidi ya Hull City iliyopigwa siku ya Jumamosi uwanjani Old Trafford na United kushinda kwa magoli 3-0, sasa mashetani wekundu wanakabiliwa na mechi zifuatazo:

Desemba 2: Stoke City
Desemba 20: Southampton
Desemba 26: Newcastle
Desemba 28: Tottenham
Januari 3 : Mechi ya mzunguko wa tatu wa FA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!