Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 December 2014
Monday, December 08, 2014

Mourinho kupumzisha Mastaa Wake




Na Florence George

Mara baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi msimu huu  dhidi ya Newcastle United timu ya soka ya Chelsea inayonolewa na Jose Mourinho sasa imeelekezea nguvu zake katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno mchezo utakaopigwa siku ya Jumatano katika dimba la Stamford Bridge.

Kuelekea mchezo huo kocha Mourinho amepanga kuwapumzisha wachezaji wake muhimu Eden Hazard,Fabregas,Thibaut Courtios na Nemanja Matic ili kuwapa nafasi wachezaji wengine ambao wamekuwa hawapati nafasi mara kwa mara.

Chelsea ambayo tayari imeshafuzu kuingia kwenye 16 bora ikishika namba moja katika kundi lake mara baada ya kufikisha pointi 11,ikifuatiwa na Sporting Lisbon yenye point 7 huku Fc Schalke 04 ikiwa na pointi 5 katika nafasi ya tatu.

Pia mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Diego Costa anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika mchezo huo ili kujiweka fiti zaidi mara baada ya siku za hivi karibuni kuwa majeruhi.

Mourinho amepanga kuwarejesha dimbani goli kipa Peter Cech,Ramires,Kurt Zouma huku John Obi Mikel akitegemewa kuanza tena katika mechi hiyo baada ya kuanza katika mechi dhidi ya Newcastle United. .

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!