Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Arsenal kumenyana na Hull City kombe la FA.




Na Florence George


Hatimae raundi ya tatu ya kombe la FA imepangwa siku ya jumatatu usiku huku Bingwa mtetezi kablu ya soka ya Arsenal ikipangwa kumenyana na klabu ya soka ya Hull City mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Emirates.

Timu zote hizo ndio zilizocheza Fainali ya kombe hilo msimu uliopita huku Arsenal ikishinda kwa magoli 3-2,shukrani kwa goli la mchezaji Aaron Ramsey katika dakika za nyongeza mara baada ya dakika 90 kumalizika huku wakiwa wamefungana magoli 2-2.

Kuelekea mchezo huo tayari kocha wa Hull City Steve Bruce amesema kuwa utakuwa ni mchezo mzuri na wa kuvutia kama ilivyokuwa fainali ya kombe hilo msimu uliopita katika dimba la Wembley.

Katika mechi nyingine klabu ya soka ya AFC Wimbledon kwa mara ya kwanza baada miaka 12 watawaarika vijana wa Brendan Rodgers timu ya soka ya Liverpool, mechi ambayo itakumbusha pambano la fainali la kombe hilo mwaka 1988 ambapo timu ya Wimbledon ilishinda kwa goli 1-0.

Klabu ya Manchester United itakuwa ikisubiri mshindi kati ya Accrington na Yeovil,huku vinara wa ligi kuu kwa sasa na mabingwa mara nne wa FA kwa misimu minane iliyopita  timu ya Chelsea yenyewe itakuwa Stamford Bridge kumenyana na Wattford iliyopo ligi daraja la pili nchini Uingereza.

Huku mabingwa wa mwaka 2011 klabu ya Manchester City itashuka dimbani katika uwanja wa Etihad kuwakaribisha timu ya soka ya Sheffield Wednesday.Mechi hizo zinajarajiwa kuanza kupigwa tarehe 3 ya mwezi january 2015.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!