Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Uchambuzi: Galatasaray vs Arsenal






Na Chikoti Cico

Uwanja wa Turk Telekom Arena uliopo jijini Instabul nchini Uturuki unatarajiwa kuwaka moto kwa kuzikutanisha timu za Galatasaray ambao ni wenyeji dhidi ya Arsenal katika moja ya mechi za kundi D za ligi ya mabingwa Ulaya.

Timu ya Galatasaray itaingia kwenye mchezo huo ili kulinda heshima tu lakini tayari wameshatolewa kwenye michuano hiyo kwani mpaka sasa inashika mkia ikiwa na alama moja hivyo ni kama watakuwa wanakamilisha ratiba tu ya mechi za kundi D.

Kocha mpya wa Galatasaray Hamza Hamzaoglu ataingia kwenye mchezo huo huku akiwakosa wachezaji wake kama Selcum Inan anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu na Blerim Dzemali ambaye ni majeruhi katika mchezo huo wa mwisho wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Rekodi ya timu ya Galatasaray dhidi ya timu kutoka Uingereza inaonyesha tangu walipofungwa mwaka 1999 na Chelsea hawajahi kufungwa tena na timu kutoka nchini humo kwenye uwanja wao wa Turk Telecom.

Kikosi cha Galatasaray kinaweza kuwa hivi: Muslera; Sarioglu, Chedjou, Kaya, Telles; Sneijder, Kurtulus, Colak, Bruma; Yilmaz, Bulut.

Kwa upande wa timu ya Arsenal wao wataingia kwenye mchezo huo ili kutafuta alama tatu muhimu na kuombea vinara wa kundi D timu ya Borrusia Dortmund kufungwa na Anderlecht ili waweze kuongoza kundi hilo, wakati huo huo kiungo wa Arsenal Alex Sanchez atapumzishwa hivyo hatacheza mchezo.

Kulekea mchezo huo kocha wa Arsenal Arsene Wenger atawakosa Theo Walcott, David Ospina, Jack Wilshere, Mesut Ozil, Mikel Arteta na Mathieu Debuchy ambao ni majeruhi huku Lukas Podolski na Joel Campbell ambao wamekuwa hawachezi mara kwa mara wakirajiwa kuwepo kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Waturuki hao.

Arsenal wataingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na takwimu za kutokuwahi kufungwa na timu kutoka Uturuki kwenye ligi ya mabingwa Ulaya huku wakiwa wameshawai kucheza na Fenerbahçe na Beşiktaş kutoka nchini humo.

Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Szczesny; Gibbs, Mertesacker, Koscielny, Bellerin; Flamini, Ramsey; Podolski, Campbell, Oxlade-Chamberlain; Welbeck.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!