Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Uchambuzi:Real Madrid vs Ludogorets Razgrad




Na Chikoti Cico



Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Ulaya timu ya Real Madrid inatarajia kuikaribisha timu ya Ludogorets Razgrad kutoka Bulgaria kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu katika moja ya mechi za kundi B za mzunguko wa mwisho wa ligi ya mabingwa Ulaya.
 
Real Madrid wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa wameshavuka hatua ya makundi baada ya kushinda mechi zote tano za mwanzo hivyo wanaongoza kundi B wakiwa na alama 15 kibindoni, kama wakishinda mchezo huo Madrid wataweka rekodi ya kucheza michezo 19 mfululizo bila kufungwa katika mashindano mbalimbali.

Pia Madrid wana rekodi nzuri kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu kwani katika michezo 19 iliyopita ya ligi ya mabingwa Ulaya wameshinda michezo 17 na kutoka sare michezo miwili bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Kocha wa Madrid Muitaliano Carlo Ancelotti kuelekea mchezo huo atawakosa Sergio Ramos aliyepewa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita, James Rodriguez na Luka Modric ambao ni majeruhi, Kikosi cha Real Madrid kinaweza kuwa hivi: Navas; Carvajal, Pepe, Varane, Marcelo; Kroos, Illarra, Isco; Bale, Benzema, Ronaldo.

Timu ya Ludogorets kwa upande wao wataingia kwenye mchezo huo kutafuta ushindi huku wakiombea Liverpool wapoteze mchezo wao dhidi ya Basel katika mechi nyingine ya kundi B itakayopigwa kwenye uwanja wa Anfield, mpaka sasa Ludogorets wanashika mkia wakiwa na alama nne kwenye msimamo wa kundi hilo.

Timu hiyo kutoka Bulgaria inaweza kumkosa mchezaji wake Mihail Alexandrov ambaye anasumbuliwa na misuli lakini Wabrazili Marcelinho na Juninho Quixada wanatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo dhidi ya Real Madrid.

Kikosi cha Ludogorest kinaweza kuwa hivi: Stoyanov; Moti, Minev, Junior, Terziev; Abalo, Dyakov, Espinho, Juninho; Marcelinho, Misidjan





0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!