Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 November 2014
Monday, November 03, 2014

Rojo nje wiki sita.


Na Chikoti Cico

Beki wa Manchester United Marcos Rojo anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki sita ama zaidi baada ya kuumia bega siku ya Jumapili kwenye mechi dhidi ya Manchester City, mchezo ulioisha kwa Manchester City kushinda kwa 1-0.

Rojo aliyesajiliwa na United kutoka Sporting Lisbon kwa kiasi cha paundi milioni 16 anaungana na Phil Jones, Jonny Evans na Rafael Da Silva ambao wote ni majeruhi hivyo kocha wa Manchester United, Luis Van Gaal anatarajiwa kumtumia kiungo Michael Carrick kama beki wa katikati kwa mechi zinazofuata.

Baada ya Chris Smalling kupewa kadi nyekundu na Marcos Rojo kuumia kwenye mchezo dhidi ya City maarufu kama “Manchester Derby” Van Gaal alimwingiza Carrick kucheza kama beki wa katikati ingawa mara nyingi huwa anacheza kama kiungo wa ulinzi.

Kuumia kwa Rojo kunaifanya beki ya United kuendelea kupata misukosuko toka kuanza kwa ligi na mpaka sasa, bado ukuta wa kocha Van Gaal haujatulia kutokana na walinzi wengi kuwa majeruhi hali inayomlazimu kutumia wachezaji chipukizi kama Tyler Blackett na Paddy McNair.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!