Steven Gerrard kuanzia benchi leo
Na Chikoti Cico
Kuelekea mechi ya kundi B ya ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia kumpumzisha nahodha Steven Gerrard.
Gerrard ambaye amecheza mechi zote za Ligi kuu ya Uingereza na Ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu, anatarajia kupumzishwa ili kuwa fiti kwenye mechi ya ligi dhidi ya vinara Chelsea itakayopigwa siku ya Jumapili. Wakati huo huo, mashabiki wa Liverpool wanatarajiwa kutokufurahishwa na uamuzi huo wa Gerrard kupumzishwa.
Akiongea na waandishi wa habari kocha Brendan alisema “ Kwa swala la Steven kama akicheza Jumamosi inabidi niangalie nini ni kipaumbele kwa ajili yake na kwaajili yetu, kama alicheza dhidi ya Newcastle na hajacheza kesho ( leo) usiku utasema hicho ndicho kipaumbele”
Brendan aliendelea kusema “Yeye (Gerrard) na mimi tumeongelea kuhusu hilo. Mechi tatu kubwa, Newcastle, Madrid na halafu Chelsea, nahitaji kuangalia namba ya wachezaji na kuangalia michezo tunayotaka wacheze” pia kocha Brendan amesema kipaumbele cha kwanza kwa Liverpool ni ligi kuu ya Uingereza halafu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kupumzishwa kwa Gerrard kwenye mchezo dhidi ya Madrid, kunatarajia kushangaza wengi na inaonekana kama ni hatari kubwa dhidi ya kocha wa Liverpool hasa ikizingatiwa kuwa Gerrard ana uzoefu wa mechi 125 za Ulaya ambazo ameweza kucheza akiwa na Liverpool.
Uzoefu ambao kwa kikosi cha sasa cha Liverpool hakuna mchezaji ambaye anao, pia kocha Brendan anaangalia uwezekano wa kumpumzisha Raheem Sterling na kuweka imani yake dhidi ya wachezaji kama Lazar Markovic na Adam Lallana.
0 comments:
Post a Comment