Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 November 2014
Tuesday, November 04, 2014

Casillas kudakia Real Madrid hadi miaka 40


Na Chikoti Cico
 
Kipa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Cassilas ambaye amekuwa akishutumiwa kwa kuonyesha kiwango kibovu kwa siku za karibuni akiongea kwenye mahojiano kabla ya mechi ya dhidi ya Liverpool amesema anataka kuichezea Real Madrid mpaka akifikisha miaka 40.

Casillas ambaye kwasasa ana miaka 33 anatarajia kufikisha michezo 144 ya ligi ya mabingwa Ulaya kwenye mechi ya Real Madrid dhidi ya liverpool itakayopigwa kwenye uwanja wa Bernabeu hivyo kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi kwenye michuano hiyo ya Ulaya.

Mpaka sasa Casillas ameweza kushinda mara tatu kombe la ligi ya mabingwa Ulaya katika miaka 15 ya kuichezea Madrid, akipingana na taarifa kwamba huu utakuwa msimu wake wa mwisho kuichezea Madrid Casillas alisema “Nafikiri naweza kucheza mpaka miaka 40, nilianzia hapa na nataka kumalizia hapa”

Baada ya Madrid kunyakua kombe la 10 maarufu kama “la decima” kwenye msimu uliopita wa ligi ya mabingwa Ulaya Casilas aongelea uwezekano wa kushinda tena kombe la 11 maarufu kama “undecima”, kipa huyo aliyeitwa kwa mara ya kwanza na Madrid mwaka 1997 akiwa na miaka 16.


Casillas aliongeza pia kuwa, Changamoto ya haraka ni kushinda kwa miaka miwili mfululizo, kama tukionyesha tamaa ile ile ya mwaka uliopita kwanini tusishinde? Kwanza tunahitaji kupita kwenye hatua ya makundi na kuwafunga iverpool itatuhakikishia hilo.

Akiongelea mchezo dhidi ya Liverpool Casillas alisema “ Liverpool wanahitaji kushinda, timu za Kiingereza kamwe hawakati tamaa, Liverpool watakuja hapa kwenye uwanja ambao wameshawahi kushinda kabla na watajitoa kwa kila kitu”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!