Raheem Sterling kuongeza mkataba Liverpool
Na Oscar Oscar Jr
Fowadi chipukizi wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Liverpool, Raheem Sterling ameahidi kukaa muda mrefu Liverpool kwa na yuko tayari kutia saini mkataba mpya, alidokeza hayo kupitia nukuu kwenye magazeti ya Uingereza siku ya Jumamosi.
Mwingereza huyo wa miaka 19 amekuwa nguzo kuu katika klabu yake na taifa katika kipindi cha miezi 12, na licha ya mwanzo mbaya wa Liverpool msimu huu, anataka kusalia Anfield.
"Nina furaha kukaa hapa muda mrefu kadiri inavyowezekana. Natumai ninaweza kupata mabao na nataka kufanikiwa nikiwa hapa Liverpool miaka mingi ijayo,” alisema Sterling, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika 2017.
Kumekuwa na taarifa nyingi kumuhusu kinda huyo kuondoka klabu hapo kutokana na kulipwa pia msharaha kiduchu wa Pauni 30,000 kwa wiki na moja ya klabu zinazotajwa kummezea mate ni mabingwa wa Ulaya, Real Madrid.
Liverpool wanataka kumuongezea mkataba mpya mchezaji huyo ambao utamfanya kulipwa mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki huku dau lake la kuuzwa kwa klabu itakayomtaka lisipungue Pauni 60M.
Sterling aliwahi kuingia kwenye mzozo kati ya klabu yake na timu ya taifa mwezi uliopita baada ya meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson alipofichua kwamba alilalamikia uchovu kabla ya mechi ya kufuzu kwa Euro 2016 ugenini Estonia.
Madai ya Hodgson yalipingwa na meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, huku baadhi ya wadadisi wa soka wakitilia shaka kujitolea kwa Sterling kuchezea timu ya taifa. Sterling alikiri kisa hicho hakikuwa cha kufurahisha, lakini akasema atajirekebisha.
0 comments:
Post a Comment