Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 November 2014
Friday, November 21, 2014

Pep Guardiola sasa kuinoa Arsenal.


Na Oscar Oscar Jr

Kila kukicha kumekuwa na taarifa zinazoashiria kufika ukomo kwa kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger. Gazeti la Daily Star leo limeripoti kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola kurithi mikoba ya Wenger ambaye amedumu na kwa klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 17.

Mashabiki wa Arsenal wameendelea kukosa amani juu ya kocha huyo ambaye licha ya kushindwa kutamba kwa siku za hivi karibuni, bado mashabiki hao wataendelea kumkumbuka kwa mengi aliyowafanyia ikiwamo Ujenzi wa uwanja mkubwa wa Emirates ambao Weger amehusika kwa kiasi kikubwa.

Arsenal wanatajwa kumchukuwa Guardiola baada ya Wenger kuondoka kwenye kiti hicho huku chagua la pili, akitajwa Muhispania mwingine, kocha Roberto Martinez ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Everton. 

Mashabiki wa Arsenal pia, wameuandikia barua Uongozi wa timu hiyo ili kusitisha upandishwaji wa tiketi za mechi msimu ujao kama kocha Arsene Wenger hatosajili mwezi January.

Pep Guardiola ambaye alishinda mataji mawili ya klabu bingwa Ulaya akiwa na klabu ya Barcelona, amewahi kusema kuwa ana ndoto za kuja kufundisha klabu inayoshiriki ligi kuu Uingereza ingawa hajawahi kubainisha klabu zinazomvutia.

Arsenal ambao wanakamata nafasi ya sita, watakuwa nyumbani Emirates Jumamosi hii kucheza na klabu ya Manchester United mchezo ambao unatarajiwa kupigwa majira ya saa 2:30 Usiku kwa saa za kwetu Afrika Mashariki.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!