YANGA ilitaka kumsainisha Jonas Mkude ikachemka dakika za mwisho baada ya Simba kumshikisha kijana Sh70 milioni na kumboreshea maisha yake.
Sasa Simba nao wamemuweka kwenye rada yao kiungo wa Yanga anayemaliza mkataba wake, Hatuna Niyonzima.
Niyonzima ameeleza waziwazi kwamba hafurahishwi na
jinsi kocha wa Yanga, Marcio Maximo anavyomtumia dakika chache na
kutomueleza lolote kuhusiana na ufanisi wake hivyo hana mpango wa
kuendelea na Yanga kama mambo yataenda kama yalivyo sasa.
Lakini Mkude baada ya kusikia Simba wanamtaka Niyonzima akawaambia: “Mtakuwa mna akili sana nyie, nileteeni jembe lile.”
Mkude ameiambia Mwanaspoti kwamba mchezaji huyo akitua Simba hali ya hewa itabadilika na kila mtu atanyamaza.
Mkude anaamini kwamba Niyonzima akitua Simba
ataongeza ushindani zaidi kwenye safi ya kiungo kwa jinsi anavyomfahamu
kwamba hana papara kwenye uamuzi wake uwanjani hivyo ni mtu sahihi kwa
Mnyama.
“Simba wakimsajili Niyonzima watakuwa wamefanya
jambo kubwa kwani ataongeza chachu ya ushindani mkubwa, hilo pia
litatufanya sisi kuwa mwiba kwa timu pinzani,kwa sababu ni mchezaji
asiye na papara pia ana uwezo wa kucheza vema nafasi hiyo,” alisema.
Source: Gazeti la Mwanaspoti
Source: Gazeti la Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment