Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 November 2014
Friday, November 21, 2014

Azam yaipa Simba dau la mwisho kwa Kiemba



KLABU ya Azam FC, imepeleka ofa ya Sh10 milioni kwa uongozi wa Simba kwa lengo la kumnasa kiungo, Amri Kiemba, kwa ajili ya kuboresha kikosi chao msimu huu.

Azam imepeleka ofa hiyo baada ya ofa yao ya awali ya kumhitaji Kiemba kwa mkopo kukataliwa, wakaambiwa wamnunue Sh15milioni.

Kiongozi wa juu wa Azam FC, ameliambia Mwanaspoti akisema: “Tumewapelekea Simba ofa ya Sh10 milioni ili watuachie, Kiemba lakini bado hawajatujibu, tunaendelea kuwasubiri waamue. 

Wakitujibu ndiyo mambo mengine yataendelea kufuata.”

Hata hivyo kulikuwa na habari za kubadilishana wachezaji kati ya mabeki wao, Said Morad au David Mwantika kwa Kiemba, lakini bosi huyo wa juu amesema jambo hilo halipo.

Azam ambayo msimu huu itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, tayari imemsainisha Muivory Coast, Pascal Wawa mkataba wa miaka wiwili na ipo kwenye mazungumzo ya kumnasa Mmali Mohamed Traole ambaye ni mshambuliaji aliyemaliza mkataba wake na El Merreikh ya Sudan.

Source: Gazeti la Mwanaspoti

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!