Kocha wa Chelsea amethibitisha kuwa mshambuliaji wake raia wa Hispania, Diego Costa sasa amepona kabisa na atakuwepo kwenye mchezo wa leo dhdi ya West Bromwich Albion kwenye dimba la Stanfford Bridge mchezo utakaopigwa majira ya saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Diego Costa ambaye alilazimika kuachwa nje na kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Vincente Del Bosque kwenye mechi mbili za kimataifa dhidi ya Belarus na Ujerumani, sasa mepona kabisa na yuko tayari kupambana uwanjani.
Chelsea ambao wanaongoza ligi kwa sasa huku wakiwa na poinri 29, leo watacheza na WBA timu ambayo imekuwa na rekodi nzuri sana ya kuwasumbua Chelsea.
Ubora wa sasa wa Chelsea, unafanya wapewe nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi hasa ukizingatia kuwa, Mourinho amepoteza mechi moja tu ya ligi kuu akiwa uwanja wa Stanfford Bridge katika maisha yake.
Kuanzia sasa mpaka mwaka mpya, Chelsea watacheza mechi 12 na huu ni mtihani kwa wachezaji wote wageni wa ligi kuu Uingereza.
Huu kwa kawaida huwa unakuwa mwezi wenye mechi nyingi sana ambapo Diego Costa naye atakuwa anaupitia kwa mara ya kwanza. Ratiba ya mechi nyingi kiasi hiki kwa kipindi kifupi, huwezi kuikuta Hispani wala Ujerumani.
Mourinho ana amini kuwa, Costa atamudu kuendana na ratiba hiyo ngumu japokuwa amebakiza kadi moja tu ya njano ili kufungiwa mechi moja.
Costa ambaye mpaka sasa amefnga mabao 10 ya ligi kuu, atahitaji kufunga goli kwenye mchezo wa leo ili kujiweka karibu na mshambuliaji wa Manchester City, Kun Aguero ambaye mpaka sasa anaongoza akiwa na magoli 12.
0 comments:
Post a Comment