Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 November 2014
Thursday, November 20, 2014

Chelsea watapata ubingwa ila watafungwa.


Na Oscar Oscar Jr

Kipa wa kimataifa wa Marekani na klabu ya Everton, Tim Howard amesema kuwa klabu ya Chelsea itatwaa Ubingwa msimu huu lakini ni vigumu kwa timu hiyo kufika mwezi Mei mwakani bila kupoteza mchezo. 

Kipa huyo ambaye hivi karibuni ametangazwa kama mchezaji bora wa mwaka nchini Marekani, amesema hadhani kama kuna timu itawazuia Chelsea msimu huu kutwaa Ubingwa.

Chelsea tayari wameshinda mechi tisa na kutoka sare mara mbili, wanaonekana moto wa kuotoa mbali msimu huu baada ya msimu uliopita kushindwa kutwaa taji lolote. 

Usajili wa kiungo Cesc Fabregas, Mshambuliaji, Diego Costa na kipa Thibout Courtois, umeleta ubora mkubwa kwenye kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho

Pamoja na timu kama Swansea City, West Ham United na Southampton kuwa ndani ya timu tano za juu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza, Tim Howard ana amini bado Everton wananafasi ya kufanya vizuri na kumaliza juu zaidi.

Everton kwa sasa wanashika nafasi ya 10 baada ya mechi 11 na kipa huyo bado ana imani kubwa kuwa timu hiyo itafanya vizuri zaidi. 

Akizungumzia safu ya Ulinzi ya Chelsea, Howard anasema huenda ni safu ngumu kupenya ambayo hajawai kuishuhudia katika ligi Uingereza huku akimsifia pia kocha, Jose Mourinho kwa kuisuka vema.

Everton baada ya mechi za kimataifa kumalizika, watakuwa nyumbani kuwakaribisha West Ham United kwenye dimba la Goodison Park kesho Jumamosi majira ya saa 12:00 Jioni  kwa saa za Afrika Mashariki. 

West Ham wamekuwa na mwanzo mzuri wa ligi kwani mpaka sasa wanakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na pointi 18.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!