Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 November 2014
Thursday, November 20, 2014

Mchezaji wa Everton anyakuwa uchezaji bora wa mwaka.


Na Chikoti Cico

Kipa wa timu ya taifa ya Marekani na klabu ya Everton ya Uingereza Tim Howard amenyakua tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka nchini marekani kwa upande wa soka (US Soccer Male Athlete of the Year) kwa mwaka 2014.

Howard ambaye ameichezea timu ya taifa ya Marekani michezo 104 na kupita rekodi ya michezo 102 iliyowekwa na kipa wa zamani wa timu hiyo, Kasey Keller amechukua tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazili mapema mwezi wa saba.

Akiongea na vyombo habari baada ya kunyakua tuzo hiyo Howard alisema “ Ni heshima, najua washindi kwenye listi ambao wamekuja kabla yangu hivyo ni maalum kwa jina langu kuwepo pale”.

"Safari yote ya timu kwa mwezi na nusu (wakati wa kombe la Dunia), wakati tulipokuwa pamoja mazoezini na tulipopaa kwenda Brazili, tulikuwa na muda mzuri na hiyo ilifanya mwaka 2014 kuwa maalum kwangu”

Kwa kunyakua tuzo hiyo zaidi ya mara moja Tim Howard anaungana na Marcelo Balboa (1992, 1994), Kasey Keller (1997, 1999 na 2005), Landon Donovan (2003, 2004, 2009, 2010) na Clint Dempsey (2007, 2011, 2012) ambao walishawahi kunyakuwa tuzo hiyo ya US Soccer Male Athlete of the Year.

Howard anayeichezea timu ya Everton ya Uingereza ambayo mpaka sasa ameichezea michezo 283 tokea alipojiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Manchester United, alishinda tuzo hiyo baada ya kuibuka kidedea kwenye idadi ya kura zilizopigwa huku akipata asilimia 64 ya kura na kuwapita Jermaine Jones aliyepata asilimia 19 na Kyle Beckermann aliyepata asilimia 11.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!