Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 November 2014
Tuesday, November 18, 2014

Benitez aishauri Liverpool.


 Na Chikoti Cico

Kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez aitaka Liverpool kuangalia mafanikio waliyoweza kuyapata msimu uliopita kwa kumaliza nafasi ya pili kwenye msimu wa ligi nchini Uingereza kama hamasa ya kuweza kufanikiwa msimu kwenye msimu huu mpya wa ligi.

Benitez ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Napoli kutoka Italia, akiongelea Liverpool ambayo kwasasa inafundishwa na kocha Brendan Rodgers alisema “Unahitaji kuwa na uzoefu kama huu na useme “nini tufanye kwasasa”.

Hatuwezi kubadilisha kilichotokea hivyo inabidi tufikirie “nini tufanye sasa kwaajili ya baadaye? Tuwe vipi kwenye nafasi ile ile? Nafikiri hicho ndicho kitu cha pekee”.

Liverpool iliwahi kumaliza nafasi ya pili ikiwa chini ya Benitez kwa msimu wa 2008/09 huku wakishinda michezo 25 na kupoteza michezo miwili tu na kutoka sare michezo 11 ambapo walimaliza wakiwa nafasi ya pili pungufu ya alama nne nyuma ya Manchester United wakati huo.

Beniteza akiongelea uzoefu wa kumaliza nafasi ya pili alisema “Tulipomaliza nafasi ya pili nlifurahia kwasababu tulikuwa na alama 86 na pia hazikutosha na kila mmoja alisema “oh ulipoteza nafasi”.

Hivyo ukiendelea kusononeka kuhusu “oh tulipoteza nafasi” hutakuwa tayari kwa yajayo. Hivyo nafikiri inahitajika kumakinika kwa ulichokifanya vizuri na ulichokifanya vibaya halafu unajaribu kuboresha kwa yajayo kwa kinachofuata”.

Wakati wa Benitez Liverpool iliweza kushinda makombe matatu likiwemo kombe la ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuifunga AC Milan kwenye fainali iliyopigwa kwenye jiji la Instanbul nchini Uturuki.

Mpaka sasa timu ya Liverpool inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 14 baada ya kushinda michezo minne, kufungwa michezo mitano na kutoka sare michezo miwili toka kuanza kwa msimu wa 2015/14.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!