KIPA AIKIMBIA TIMU YAKE WAKATI IKIPASHA UWANJANI.
Na Oscar Oscar Jr
Jumapili wikendi iliyopita kulikuwa na mchezo wa kufuzu kwa mataifa ya Ulaya, maarufu kama Euro 2016 uliochezwa kwenye dimba la Turk Telekom jijini Instanbul, uwanja ambao hutumiwa na miamba ya soka nchini humo, timu ya Galatasaray.
Uturuki walikuwa wanacheza na timu ya Kazakhstan na wakati timu zikipasha misuli, ndipo mashabiki wanaosadikiwa kuwa wa Galatasaray, walianza kumporomoshea matusi kipa wa Urusi,
Volkan Demirel ambaye anadakia klabu pinzani ya Fenerbahce.
Baada ya golikipa Demirel kuona matusi yamezidi, aliamua kumfuata kocha wake wa timu ya taifa, Fatih Terim na kumwambia kuwa ameshindwa kuvumilia matusi ya nguoni kutoka kwa mashabiki hao na hivyo anaomba atoke nje ya uwanja.
“Bibi na watoto wangu pia hawawezi kepuka matusi haya ya laana. Sina roho ya kucheza mbele ya watu ambao wanarusha maneno machafu sana. Nitakiathiri kikosi badala ya kukisaidia,” alinukuliwa golikipa huyo kabla ya kutoka zake nje ya uwanja.
Kipa wa ziada, Volkan Babacan alichukua mahala pake na Uturiki walifanikiwa kujipatia ushindi wa 3-1 na kunusuru hadhi yao baada ya kucharazwa 4-0 na Brazil mapema mwezi huu katika mchezo wa kirafiki.
Ingawa hatua za kinidhamu zinaweza chukuliwa dhidi ya Demirel, kocha Terim amepuuzia kisa hicho akisema ni mapema sana kukimbilia uamuzi.
0 comments:
Post a Comment