Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 February 2017
Thursday, February 02, 2017

TUANZEBE ASAINI MANCHESTER UNITED



Na FLORENCE GR 

Mchezaji chipukizi wa Manchester united Aet Tuanzebe amefanikiwa kuongeza mkataba wa miaka mitatu na nusu kuendelea kuichezea kablu  hiyo ikiwa ni baada ya siku kadhaa kufankiwa kuicheza kwa mara ya kwanza katika michuano ya FA dhidi ya Wigan katika uwanja wa Old Traford.

Mchezaji huyo mweye umri wa miaka 19 ataendelea kuichezea timu hiyo hadi mwaka 2020 huku klabu ikiwa na uwezo wa kuongezea mkataba mwingine kwa miaka kadhaa ijayo.

Akiongea kupitia website ya timu Tuanzebe alisema kuwa 'Nimekuwa mshabiki wa Manchester united asilia kwahiyo najisikia furaha kusaini mkataba mpya'.aliongeza kuwa 'kucheza kwenye uwanja wa Old Traford kwenye mechi ya FA ilikuwa fahari sana kwangu na familia yangu'.

'Nimekuwa nikijfunza kila siku mazoezini na ni uzoefu mkubwa kubwa kufanya mazoezi na timu ya kwanza, napenda kuwashukuru makocha wote niliofanya nao kazi na shukrani za pekee ziende kwa kocha wangu kwa kinipa nafasi ya kucheza katika timu hii'.

Akiongelea kuhusu kuongeza mkataba kwa mchezaji huyo kocha wa united Jose Mourinho anasema kuwa' Axel ni kijana mdogo mwenye kipaji kikubwa, tulimuweka timu ya kwanza ili kumuongezea uzoefu na alifanikiw kweli'.

'Nina furaha kwamba amesaini mkataba mpya na ninafurahia jinsi anavyoendelea' alimalizia kwa kusema hivyo kocha Mourinho ambae jana ilishuhudiwa timu yake ikitoka sare ya 0-0 dhidi ya Hull city katika dimba la Old Traford.

Axel amekuwa united na tangu alipoingia kwenye Academy ya timu hiyo alipokuwa na umri wa miaka minane.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!