Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 February 2017
Friday, February 03, 2017

PIRES:TUKIFUNGWA TENA UBINGWA BASI


Na FLORENCE GR

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa na Arsenal Robert Pires anaamini kuwa mbio za ubingwa wa ligi kuu Uingereza  kwa upande wa Arsenal zitafikia ukomo kama Arsenal watakubali kipigo kutoka kwa chelsea siku ya kesho.

Arsenal wanazidiwa pointi tisa na Chelsea ambao ni vinara wa EPL  ambao katika mechi iliyopita walitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Liverpool huku Arsenal akifungwa goli 2-1 dhidi ya Watford. 

Pires ambae alifanikiwa kushinda mataji mawili ya EPL akiwa anaichezea Arsenal amewaambia waandishi wahabari kuwa Arsenal inahitaji kupata matokeo mazuri Stamford bridge ili kuendelea kuweka matumaini ya ubingwa.

'Itakuwa ngumu mechi ngumu sana baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Watford, lakini tuna nafasi nyingine siku ya jumamosi, kwangu mimi hii ni kama fainali ya EPL, kama Chelsea ikiifunga Arsenal  basi ligi itakuwa imeisha'.

'Chelsea wana timu nzuri , wanacheza vizuri, wanacheza kwa umoja na wana falsafa ya kitaliano wagumu kufungika' alisema Pires.

Naye beki wa zamani wa Chelsea Marcel Desailly anakubaliana na Pires ili kuendelea kupigania ubingwa Arsenal wanahitajika washinde mchezo huo.

Deasailly anasema kuwa 'kama unafungwa na Watford ni vigumu kuwa na mawazo ya kushinda moja kwa moja ugenini dhidi ya Chelsea'.

'Kwa Chelsea sio muhimu sana, timu inajiandaa kwa mchezo kama michezo mingine, ni mechi muhimu kwasababu ni derby lakini sio kitu muhimu kushinda au kufungwa kitu cha msingi ni kuendelea na kiwango kizuri hadi mwisho mwa msimu' alisema Deasailly.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!