Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 February 2017
Thursday, February 02, 2017

SOUTHAMPTON YAPATA PIGO

Na FLORENCE GR

Klabu ya soka ya southampton imedhibitisha kuwa beki wake raia wa uholanzi Virgil van Dijk atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili hadi mitatu baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipata majeraha hayo baada ya kugongana na mshambuliaji wa Leicester city Jamie Vardy katika ushindi wa goli 3-0 ambao southampton iliupata.

Mchezaji huyo amabye amekuwa nguzo muhimu msimu, ameanza katika mechi 30 msimu huu na kufunga magoli manne  anatarajia kukosa mechi ya fainali ya kombe la ligi dhidi  manchester united mchezo unaotarajiwa kupigwa mwezi huu.

Southampton walifanikiwa kutinga fainali ya kombe la ligi baada ya kuifunga klabu ya liverpool kwa jumla ya magoli 2-0 katika mechi mbili  walizokutana.




0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!