Na FLORENCE GR
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na Chelsea Frank Lampard ametangaza kustaafu kucheza soka rasmi na kugeukia mafunzo ya ukocha yanayatolewa na chama cha soka cha Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye msimu uliopita alikuwa akikipiga katika timu ya New York City inayoshiriki liki kuu Marekani(MLS) ametangaza uamuzi huo kupitia mtandao wake wa kijamii .
Lampard anasema kuwa' nimepokea ofa mbalimbali ya kuendelea kucheza, kwa umri wa miaka 38 sasa ni muda wa kuanza ukurasa mpya wa maisha yangu'.
'Nashukuru sana chama cha soka kwa kwa nafasi hii ya kujifunza mafunzo ya ukocha'
Katika kipindi cha maika 13 aliyoitumikia Chelsea Lampard amefanikiwa kuichezea mechi 649 na kufunga magoli 211 amabayo yanamfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo huku akifanikiwa kuichezea timu ya taifa ya Uingereza mechi 106.
Lampard alijiunga na Chelsea akitoa timu ya west ham mwaka 2001 kwa kiasi cha euro million 11 na kufanikiwa kutwaa mataji 11 tofauti tofauti ikiwemo klabu bingwa ulaya mara moja ,FA cup(4), kombe la ligi (2),europa ligi mara moja na EPL mara 3.
Zifuatazo ni rekodi mbalimbali za Frank Lampard;
- Lampard ni mchezaji wa tatu aliecheza mechi nyingi za ligi kuu uingereza nyuma ya Ryan Giggs aliecheza mechi 632 na Gareth Barry aliecheza mechi 609.
- Lampard amefunga magoli 177 katika ligi kuu Uingereza na kushika namba nne kwenye orodha ya wafungaji wenye magoli mengi nyuma ya Alan Shearer, Wayne Rooney na Andy Cole.
- Lampard ndio mchezaji anaeongoza kwa kufunga magoli mengi nje ya eneo la penati box katika ligi kuu uingereza magoli 41.
- Lampard amezifunga timu 39 tofauti kwenye ligi kuu uingereza
- Hakuna mchezaji wa uingereza aliefunga penati nyingi zaid ya Lampard (9)
0 comments:
Post a Comment