NANI KUCHEZA FAINALI NA MISRI?
Na FLORENCE GR
Mchezo wa nusu fainali ya pili unatarajiwa kupigwa leo nchini Gabon ambapo mashindoni ya AFCON yanaendelea kupamba moto kwa kuwakutanisha mabingwa mara nne wa kombe hilo timu ya Ghana dhidi ya Cameroon katika dimba la Stade de Franceville.
Ghana ambao walipoteza katika mchezo wa fainali wa AFCON iliyopita nchini Equatorial Guinea kwa kufungwa na Ivory cost kwa mikwaju ya penati wataingia uwanjani kwa nia ya kutafuta tiketi ya kuelekea fainali ambapo tayari timu ya Misri imeshafuzu.
Cameroon ambayo ilikuwa haipewi nafasi kutokana na kikosi chake kuwa na wachezaji vijana na wasio na majina walishanga watu pale walipoitoa Senegal kwa mikwaju ya penati 5-4 kwenye hatua ya robo fainali huku Senegal iliyokuwa na wachezaji nyota wengi na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe hilo.
Kikosi cha Cameroon kinaonekana kuimalika mechi baada mechi huku wakijivunia goli kipa wao Fabrice Ondoa ambaye amekuwa katika kiwango cha hali ya juu katika michuano hiyo na kutegemewa kuivusha timu hiyo hadi fainali tangu mwaka 2008.
Cameroon walitwaa ubingwa huo mwaka 2002 nchini Mali huku Ghana walitwaa kwa mara ya mwisho mwaka 1982 nchini Libya zitaingia uwanjani zikiwa na hasira ya kila mmoja akihitaji kuchukua kwa mara ya tano kombe hilo kwenye fainali itakayopigwa tarehe 5 February kwenye uwanja wa Stade de l'Amitié.
Ghana inatarajia kukosa huduma ya nahodha wao Asamoah Gyan kwa mechi ya pili mfulilizo ambae bado hajapona majeruhi aliyopata katika mchezo wa mwsiho wa makundi dhidi ya Misri.
Huku Vincent Aboubakar wa cameroon ambae amekuwa akianzia benchi katika mashindano haya akitarajia kuanza kwenye mchezo huo.
Ghana wataingua uwanjani wakiwa na matumaini kwa Andre na Jordan Ayew ambao walifanikiwa kufunga kwenye mchezo wa nusu fainali huku Cameroon wakimtegemea goli kipa wao ambao alifanikiwa kuokoa michomo mitatu dhidi ya Senegal kabla ya kupangua penati ya Saido Mane na kuwavusha hadi nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment