Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 February 2017
Friday, February 03, 2017

AGUERO BADO ANAFURAHA MAN CITY- HERNAN REGUERA


Na FLORENCE GR

Wakala wa mshambuliaji wa Manchster City Sergio Aguero amepuuzilia mbali taarifa zilizosambaa kuhusiana na mteja wake kutakiwa na matajiri wa Hispania Real Madrid katika dirisha la usajili wa majira ya joto.

Kumekuwa na maswali mengi sana juu ya mustakabali waAguero kwenye timu hiyo baada ya kocha wa City Pep Guardiola kumuweka benchi staa huyo na kumpa nafasi Gabriel Jesus amabe amejiunga na timu hiyo siku za hivi karibuni katika ushindi wa magoli 4-0 walioupata dhidi ya West Ham .

Aguero ambae ameshafunga magoli 11 katika michezo 17 ya ligi kuu msimu huu aliingia kama mchezaji wa akiba katika kipigo cha magoli 4-0 walichopata dhidi ya Barcelona mwezi October na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burnley mwezi uliopita huku Guardiola akitoa sababu na kusema kuwa bado anahitaji kuona mambo mengi zaidi kutoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.

Gazeti la Dairy Mirror siku ya ijumaa liliripoti kuwa Real Madrid wanajiandaa kupeleka ofa ya kumtaka mchezaji huyo  majira ya kiangazi huku klabu za Juventus, PSG na Athletico Madrid zikitajwa kumfatlilia kwa karibu muargentina huyo.

Hernan Reguera ambae ni wakala wa mchezaji huyo amelazimika kutolea ufafanuzi na kusema kuwa ' Aguero anafuraha sana na anatarajia kuwepo hapa msimu ujao'.

Akiongeleza kuhusu swala la Aguero kutoelewana na Jesus,Hernan amesema kuwa 'hakuna tatizo lolote baina yao juu ya kushindania namba ya kuanza katika mchezo'.

Jesus ambae aliwasili katika klabu hiyo mwezi uliopita baada ya kukamilisha taratibu ya usajili kutoka Palmeiras ameanza kuonyesha cheche zake katika ligi hiyo baada ya kuingia dakika za mwishoni kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham na kuonyesha kiwango kizuri huku akianza kwenye michezo miwili iliyofuata na kutoa pasi ya goli katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Crystal Palace na kufunga goli moja dhidi ya West Ham United.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!