Na FLORENCE GR
Klabu za jiji la Manchester zimefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao iliyocheza hii leo katika ligi kuu ya nchini uingereza ambapo katika dimba la Etihad Vijana wa Pep Guardiola walifanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Swansea city huku Manchester united ikiibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya mabingwa watetezi Leicester city.
Ilimchukua dakika 11 tu kwa Gabriel Jesus kuifungua Man city na kuiweka mbele dhidi ya Swansea chini ya Paul Clement ambao wanaonekana kuimarika siku hadi siku.
Manchester city walitawala mpira katika kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili Swansea ilionekana kuimarika kiasi na dakika ya 81 Sigurdsson kuisawazishia timu yake na kuonekana kama wangeweza kuondoka na pointi katika uwanja wa Etihad lakini alikuwa ni Jesus tena alieihakikishia city pointi tatu baada ya kufunga goli la pili dakika za mwishoni mwa mchezo huo.
Kwa upande hali bado si nzuri kwa mabingwa watetezi Leicester city baada ya kukubali kipigo kingine toka kwa manchester united cha magoli 3-0 katika uwanja wa King Power.
Mkhitaryan ameendelea kuonyesha thamani ya kusajiliwa na Manchester united baada kufunga goli moja na kutengeza lingine na hivyo kupelekea tofauti ya kutafuta namba nne kubaki pointi mbili.
Baada ya kutoa sare tatu mfululizo kwenye michezo ya ligi kuu kocha wa Manchester united Jose Mourinho alilazimika kubadili mfumo wa uchezaji kutoka 4-1-4-1 hadi 4-4-2 huku akimuweka nje Mihael Carrick na nafasi yake kuchukuliwa na mhispania Juan Mata.
Hata hivyo united walionekana kutokuwa kwenye kiwango kizuri na kulazimu kubadili mfumo na kucheza 4-2-3-1 Mkhitaryan akicheza namba 10 nakuanza kuifungua balo dakika 42 baada ya kumpita beki Robert Huth.
Iliwachukua united si chini ya sekunde 90 kuongeza goli la pili lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic akiunganisha krosi iliyopigwa na Antonio Valencia.
Mata alihitimisha idadi ya magoli dakika ya 49 baada kuchezeana 'one-two' safi na Mkhitaryan na kuifanya United kufikisha pointi 45, pointi moja nyuma ya Liverpool waliopo nafasi ya tano na pointi mbili nyuma ya Arsenal waliopo nafasi ya nne na kuendelea kushika nafasi ya sita ambayo wamekaa tangu mwezi November mwaka jana .
Manchester city wenyewe wamepanda hadi nafasi ya tatu wakifikisha pointi 49 na kuishusha Arsenal wenye alama 46 baada ya jana kukubali kipigo cha 3-0 toka kwa vinara Chelsea wenye pointi 59.
0 comments:
Post a Comment