MANCHESTER UNITED YAMREJESHA KIPA WAKE
Na FLORENCE GR
Manchester united imemuita goli kipa wake mwenye umri wa miaka 19 Dean Henderson kutoka klabu ya Grimsby Town ambapo alikuwa anacheaza kwa mkopo baada ya goli kipa wake chaguo la tatu Joel Pereira kupata majeruhi.
Henderson alijiunga na Grimsby town majira ya joto msimu uliopita kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita kaba ya kuongeza na kuendelea kuichezea timu hiyo ya daraja la pili hadi mwisho mwa msimu .
Pereira aliingia kutoka benchi kwenye ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Wigan kwenye mchezo wa FA wiki iliyopita alipata majeruhi mazoezini hivyo kuwalazimu mabingwa hao wa kihistoria wa uingereza kukatisha mkataba wa mkopo wa Henderson.
Henderson ambaye tayari ameshaichezea timu hiyo sasa anaweza kujumuisha kwenye kikosi na kocha Jose Mourinho kuelekea mchezo wao dhidi ya Leicester city kama akihitajika.
Henderson ameanza katika mechi saba za Grimsby kwa misimu miwili kwenye ligi daraja la pili,kufanikiwa kutofungwa kwenye mechi tatu kati ya nne aliyocheza mwezi January mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment