FAINALI YA UEFA 2019 KUCHEZWA BAKU AU MADRID
Na FLORENCE GR
Shirikisho la soka barani ulaya UEFA limetangaza viwanja viwili ambayo vitaingia katika mpambano na kupatikana kiwanja kimoja ambapo fainali ya UEFA mwaka 2019 itafanyika ,viwanja hivyo ni Bakus Olympic uliopo nchini Azerbaijan na uwanja Estadio Metropolitano ambao ni uwanja mpya wa Athletico Madrid ambao wataanza kuutumia msimu ujao.
UEFA inatarajia kutangaza mmoja wa viwanja hivyo mwezi September huku uwanja wa Baku ukipigiwa chepuo ya kuandaa fainali hiyo na kama endapo utafanikiwa itakuwa ni mara ya kwanza fainali ya UEFA kuchezwa nchini Azerbaijan .
Mara ya mwisho mji wa Madrid kuandaa fainali ya UEFA ilikuwa mwaka 2010 ambapo Jose Mourinho akiingoza Inter Milan na kufanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuifunga Bayern Munich magoli 2-0 katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu.
Baku pia imechaguliwa tena katika kuandaa fainali ya Europa ya mwaka 2019 ambapo inashindania na majiji ya Tbilisi, Glasgow, Frankfurt, Stuttgart, Istanbul na Sevilla lakini haiwezi kuchaguliwa kuandaa fainali mbili hivyo endapo itachaguliwa moja kati ya hizo basi fainali nyingine itaandaliwa na nchi nyingine.
Fainali ya UEFA mwaka huu inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Cardiff nchini Wales huku Europa itachezwa katika jiji la Stockholm nchini Sweden.
0 comments:
Post a Comment