FIRMINO ALIMWA FAINI-ENGLAND
Na FLORENCE GR
Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anaekipiga katika timu ya Liverpool Roberto Firmino amepigwa faini ya euro 20,000 na kupigwa marufuku kuendesha gari kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kuendesha gari huku akiwa amelewa siku ya krismasi.
Michael Hogan ambaye ndio alikuwa akimtetea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alisema kuwa Firmino alifanya tukio hilo siku moja baada ya familia ya mwanasoka huyo kuwa walengwa wa kuvunjiwa nyumba na vibaka ambao walikuwa wamepanga kutumia nguvu yingi.
Akiongea baada ya kutoka mahakamani Firmino amesema kuwa ' naomba msamaha bila kusita kwa klabu,kocha , wachezaji wenzangu na mashabiki kwa kujiweka katika hali hii. kwa kile nilichofanya nilikosea na ni mfano mbaya'.
Firmino pia ameomba msamaha kwa mwanafamilia yoyote yule wa klabu huku akisema atajifunza kutokana na kosa hilo huku akiahidi kutorudia kufanya kosa kama hilo tena .
0 comments:
Post a Comment