Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2017
Wednesday, February 01, 2017

HAZARD: NI MAN UNITED NA ARSENAL NDO WAPINZANI WETU TU






Na FLORENCE GR

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubeligiji na timu ya chelsea Eden Hazard amesema kuwa anaamini timu za manchester united na Arsenal ndo zinauwezo wa kuwakimbiza katika kuwania ubingwa wa Uingereza.

Hazard ameongea hayo mara baada ya kukutana na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo katika kituo cha sky sport na kocha msaidizi katika timu ya taifa ya Ubeligiji.

Chesea wanaizidi Arsenal pointi tisa ambao ipo nafasi ya tatu na pointi 15 dhidi ya manchester united iliyopo nafasi ya sita, huu  wakitarajia kukutana na Arsenal weekendi hii katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu katika uwanja wa stamford bidge baada ya kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa mwaka jana katika dimba la Emirates.

Hazard alisema kuwa' united walikuwa na wakati mbaya ndani ya kipindi kifupi cha msimu lakini kwa michezo kadhaa sasa wanacheza vizuri, walitoa sare dhidi ya stoke city lakini wana kikosi kizuri, wachezaji wazuri hata kocha wao mzuri pia hivyo watakuwa wa pili au watatu msimu huu'.

Hazard ambae amefundishwa na kocha wa sasa wa manchester united Jose Mourinho kwa muda wa miaka miwili na nusu na kufanikiwa kuchua ubingwa wa EPL mara moja mwaka 2014/2015 kabla ya mreno huyo kufukuzwa msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa italia Antonio Conte kunako majira ya joto mwaka jana.

Pia Hazard ameelezea utofauti jinsi alivyokuwa akicheza chini ya Mourinho na Conte ambapo amesema kuwa 'nikiwa na Mourinho Nemanja Matic alikuwa akicheza nyumba nyangu msimu ambao tulishinda ubingwa'.

'Lakini chini ya Conte mambo ni tofuti kabisa kwani sasa hivi nasongea ndani sana kwa sababu Marcos Alonso anacheza kama wing-back, hivyo nahitaji kusubiri mipira kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza '.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!