Utata
umeibuka juu ya jezi mpya za Newcastle kutoka kwa wadhamini wao
kutokana na mshambuliaji wake nyota, Papiss Cisse ameshautaarifu uongozi
wa klabu hiyo kwamba hatovaa tangazo la Wonga.com.
Mshambuliaji
huyo wa Senegal ni muumini safi wa dini ya Kiislamu na aliwataarifu
mapema viongozi wa klabu hiyo juu ya kutokuwa tayari kwenda kinyume cha
maadili ya dini yake kwa kutangaza biashara za kampuni hiyo ya mikopo.
Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, waumini wa dini hiyo hawaruhusiwi
kunufaika au kujinufisha na riba kutoka kwa mtu mwingine. Benki za
Kiislamu hazitoi riba.
Wachezaji wenzake CIsse, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa, ambao pia ni Waislamu, nao pia wanaweza kugoma kuvaa jezi hizo.
Newcastle haiko tayari kuachana na mchezaji huyo na wanaweza wakafanya
kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Tottenham na West Ham,
Freddie Kanoute.
Mmali huyo aligoma kuvaa jezi ya nembo ya tovuti ya 888.com alipokuwa Seville miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya kamari.
Kanoute alishikilia msimamo wake na hakuvaa nembo hiyo kwenye mashindano ya Hispania, ingawa mazoezini alikubali kuvaa.
Baadaye alikubali kuvaa kwa masharti ya kutotumika katika matangazo yoyote ya kibiashara.
Wonga, ambao udhamini wao wa miaka minne unaanza msimu ujao, tayari
inakabiliwa na zengwe lingine katika masuala ya utozaji wa riba za
mikopo yake.
Inasemekana mmiliki wa klabu hiyo anafikiria kumuuza
mshambulizi huyo kwa klabu ya Russia ili asipoteze dili lake hilo nono
na Wonga.
Wonga watapunguza pesa watakazoilipa klabu hiyo kama mmoja wa wachezaji hatovaa nembo yao.
0 comments:
Post a Comment