NYOTA wa Brazil, Neymar amemtaka
mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kufikiria kuhamia
Barcelona, akisema itakuwa ni ndito kucheza na mshambuliaji huyo wa
England.
Neymar, ambaye mwenyewe amejiunga na
timu hiyo ya Katalunya mapema majira haya ya joto kwa dau la Pauni
Milioni 48.6 kutoka Santos ya Brazil, ameitaja Camp Nou kama kituo
sahihi kwa mchezaji mwenye kipaji kama Rooney.
Nyota huyo wa Samba, aliyefunga bao tamu
wakati Brazil ikiichapa 3-0 Hispania jana katika Fainali ya Kombe loa
Mabara, amesema: "Mtindo wa soka tunaocheza (Barcelona) na viwango vya
wachezaji tulionao- ni klabu sahihi kwa wachezaji wakubwa kujiunga
nayo,".
Nyota: Neymar alitoa mchango mkubwa kwa Brazil kutwaa Kombe la Mabara
Neymar akiwatoka mabeki wa Hispania jana
Wayne Rooney atakuwa na mazungumzo na kocha mpya David Moyes kesho juu ya mustakabali wake Man United
Dream Team: Neymar na Lionel Messi wataongoza safu ya ushambuliaji ya Barcelona msimu ujao
0 comments:
Post a Comment