MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amewasili
kukutana na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes juu ya
mustakabali wake katika klabu hiyo asubuhi ya leo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27
hakuonekana aliye vizuri wakati anaendesha gari lake aina ya Range Rover
Rover ambalo kwa Tanzania wanatumia matajiri kama Yussuf Bakhresa wa
Azam, Yussuf Manji wa Yanga na Zacharia Hans Poppe wa Simba, katika eneo
la Uwanja wa mazoezi vya United majira ya saa 3.30 asubuhi, sawa na
tano kwa Dar es Salaam.
Amekutana na kocha Moyes kujadili
mustakabali wake baada ya kupoteza mawasiliano na Sir Alex Ferguson
msimu uliopita. Rooney aliondoka Carrington saa 6.45 mchana, sawa na saa
nane kwa Tanzania.
uso wa mbuzi: Wayne Rooney akiwasili Uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington na Range Rover lake la rangi ya fedha
Mkutanoni: Anakwenda kukutana na David Moyes
Kwa mitindo: Rooney akiendesha gari maeneo ya Carrington
Kocha naye: Moyes naye aliwasili Carrington mapema tu saa 1.30 asubuhi leo
Huyu anafurahi kurejea kazini: Rio Ferdinand akiwasili Carrington leo mwenye furaha tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya
0 comments:
Post a Comment