Hatarii,Cristiano Ronaldo hapatikani kirahisi
Na Florence George
Jorge Mendes amabaye ni wakala wa nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amesema kuwa mchezaji huyo atapatikana kwa kiasi cha Euro Millioni 300 kama timu yoyote inayohitaji huduma ya mchezaji huyo.
Ronaldo alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea klabu ya Manchester United kwa kiasi kilichoweka rekodi ya usajili cha Euro millioni 80 na mpaka sasa amefanikiwa kuchukua tuzo mbili mfululizo za mchezaji bora wa dunia(FIFA Ballon d'Or).
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa kwa siku za hivi karibuni kurejea Old Trafford japo kuwa anamkataba na timu hiyo hadi mwaka 2018 lakini Mendes alizionya timu zote zinazomnyemelea mchezaji huyo kuwa ziandae dau kubwa la kumpata nyota huyo.
Mendes aliiambia BBC Sport pale alipoulizwa Gharama ya kumpata mchezaji huyo alisema kuwa "kama kutakuwa na sababu yoyote itakayomfanya auzwe katika klabu basi atauzwa kwa dau la Euro millioni 300 na atakuwa tayari kucheza katika timu hiyo".
Mendes aliendelea kusema kuwa Ronaldo ni mchezaji bora kwa sasa na huwezi kumlinganisha na mchezaji yoyote yule.
0 comments:
Post a Comment