UCHAMBUZI: LIVERPOOL VS CHELSEA
Na FLORENCE GR
Mwezi january haukuwa mwezi mzuri kabisa kwa klabu ya soka ya liverpool na Jurgen Klopp mwenyewe, tangu walipofanikiwa kuifunga Manchester city goli 1-0 tarehe 31 december 2016 klabu ya liverpool imefanikiwa kushinda mechi moja tu kati ya nane iliyocheza mwezi january, mechi ya marudiano dhidi ya timu daraja la nne Plymouth goli 1-0 baada ya ile wa awali kuisha kwa sare ya bila kufungana.
Sare mbili na kipigo kimoja kimeifanya klabu hiyo kuwa nyuma ya Chelsea ambao ni vinara wa EPL kwa tofauti ya pointi 10, huku ikishuhudiwa ikitolewa nje katika kombe la ligi na FA ndani ya siku tatu huku wakitolewa mbele ya mashabiki wao kunako uwanja wa Anfield.
Liverpool amabayo haijawahi poteza michezo minne mfululizo katika uwanja wa nyumbani tangu msimu wa 1923-24 usiku wa leo itakuwa na kibarua kigumu pale itakapovaaana na vinara wa ligi hiyo timu ya Chelsea ambayo inaonekana ipo katika kipindi kizuri cha ushindi.
Chelsea wataingia uwanjani hapo wakiwa na kumbukumbu wa kufungwa goli 2-1 ktika mchezo wa awali uliopigwa miezi kadhaa iliyopita katika dimba la Stamford bridge hivyo hawataka kufanya makosa kama yale yaliyotokea katika mchezo wa awali.
Liverpool amabao wamecheza si chini ya mechi tatu zaidi ya chelsea mwezi huu-mechi mbili za nusu fainali ya kombe la ligi na mechi moja ya marudiano dhidi ya plymouth huku kwa kiasi kikubwa pengo la nyota wa kimataifa wa Senegal Saido Mane kuonekana kushindwa kupata mtu sahihi wa kuliziba hivyo kuilazimu kumtumia ndege binafsi nyota huyo mara baada ya timu yake kutolewa robo fainali ya michuano ya AFCON inayoendelea nchini Gabon.
Beki wa kulia wa liverpool Nathaniel Clyne anatarajia kukosa mchezo huo hali ambayo itaendelea kutoa nafasi kwa kijana mdogo Alexander-Arnold kucheza mchezo huo huku Adam Lallana na Roberto Firmino wakitarajia kurudi kikosi cha kwanza usiku wa leo.
Ili kuendelea kufufua matumaini yao ya ubingwa kuendelea kuwa hai liverpool leo watahitajika kushinda mchezo huu lakini pia kuhakikisha wanabaki katika nafasi nzuri ndani ya nne bora kwani wapinzani wao Arsenal, manchester city, Tottenham na Manchester united wanatazamiwa kukuibuka na ushindi katikati ya wiki hii.
Kwa upande wa Chelsea ambayo inaonekana wiki hii itakuwa ngumu kwao kwani baada ya mechi hii watarudi uwanja wa nyumbani kuwasubiri wabeba mitutu wa London Arsenal, hawana majeruhi yoyote yule hivyo kutoa nafasi kwa muitaliano Antonio Conte kurudisha kikosini wachezaji wote waliopumzisha katika mechi dhidi ya Brentford wiki iliyopita kwenye kombe la FA.
Chelsea imeshinda mechi moja kati ya sita za hivi karibuni dhidi ya Liverpool ambapo mara ya mwisho kucheza Anfield timu hizo zilitoka sare ya 1-1 huku Eden Haard akifunga "a wonderful goal" katika mechi hiyo.
Mark Clattenburg anatarajiwa kuwa mwamuzi wa mchezo huo ukiwa ni wa pili kwa chelsea kuchezeshwa na mwamuzi huyo mara baada wa ule dhidi ya Burnely mwezi August na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0.
Mpaka sasa msimamo wa ligi kuu Uingereza unaonyesha kuwa Chelsea anaongoza ligi kwa kuwa na pointi 55, akifuatiwa na Arsenal mwenye pointi 47 huku Tottenham akiwa nafasi ya tatu akiwa na pointi 46 na nafasi ya nne ikishikiliwa na Liverpool wenye pointi 45 wote wakiwa wamecheza mechi 22.
0 comments:
Post a Comment