DEMBA BA AREJEA UTURUKI TENA
Na FLORENCE GR
Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle united na chelsea Demba ba amreejea kunako timu ya Besiktas ambayo aliondoka mwaka 2015 na kwenda kujiunga na timu ya Shanghai shenhua ya nchini china baada ya kufanikiwa vipimo vya afya alivyofanya siku ya jumatatu.
Msambuliaji huyo wa kimataifa Senegal ana umri wa miaka 31sasa na alifanikiwa kufunga magoli 14 katika mechi 18 alizoichezea Shanghai mwaka 2016 kbla ya kuvunjika mguu kwenye mechi dhidi ya Shanghai SIPG ambao ndio wapinzani wao wakuu mwezi july.
Demba Ba alikaa nje ya uwanja kwa kipindi cha msimu
kilichokuwa kimebaki lakini bado alifanikiwa kumaliza namba kwenye orodha ya wafungaji wa ligi hiyo nyuma ya mbrazili Ricardo Goulart anayecheza kwenye timu ya Guangzhou Evergrande.
Tangu arejee kutoka kwenye majeruhi Ba bado hajacheza mechi yoyote ile ya ushindani huku nafasi yake ndani ya Shanghai ikiwa kwenye hati hati mara baada ya timu hiyo kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Carlos Tevez kwa mkataba wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment