Na FLORENCE GR
Mwaka 2017 unaonekana kuanza vibaya kwa klabu ya liverpool 'majogoo wa jiji' kwani katika michezo minane waliyocheza mwaka huu wameibuka na ushindi katika mchezo mmoja tu mechi dhidi ya Plymouth argyle huku wakitoa sare mechi tatu na kufungwa mechi nne.
Baada ya katikati ya wiki hii kushudiwa timu hiyo ikisukumizwa nje ya mshindani ya EFL CUP baada ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya southampton katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali katika dimba la Anfield, timu hiyo imesukumizwa tena nje ya mashindano ya FA CUP baada ya kukubali kipigo tena Anfield cha magoli 2-1 kutoka kwa wolverhampton wanderes.
Katika mchezo huo kocha wa liverpool Jurgen Kloop alifanya mabadiliko mengi kwenye kikosi chake kwa kupumzisha nyota wake muhimu kwa ajiri ya mehi ijayo dhidi ya vinara wa EPL chelsea huku roberto firmino na Loris Karius pekee wakianza toka kwenye kikosi kilichofungwa 1-0 na southampton katikati ya wiki.
Richard Stearman ndo alikuwa wa kwanza kutumbukiza mpira kimiani kwa kichwa langoni wa liverpool katika dadika ya kwanza tu ya mchezo mara baada ya free kick nzuri kabla ya Andreas Weimann kufunga goli la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku liverpool wakilishambulia kwa kasi lango la Wolves lakini ukuta wa timu hiyo ulikuwa imara na kuondosha hatari zote hata hivyo liverpool walipata goli la kufutia machozi dakika ya 86 kupitia kwa mbeligiji Divock Origi hivyo hadi dakika 90 zinaisha liverpool 1- 2 wolves.
Vinara wa EPL chelsea imeendelea kutoa vipigo vikali mara baada ya kuifunga timu ya Brentford goli 4-0, huku vijana wa Pep Guardiola Manchester city kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Crystal palace .
Totenham hotspurs iliwalazimu kusubiri hadi dakika za majeruhi kuibuka na ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Wycombe huku shukrani kwa goli la Heung-min son kunako dakika ya mwisho kabisa ya mchezo.
0 comments:
Post a Comment