Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 January 2015
Sunday, January 04, 2015

Manchester United yapiga mtu.



Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kuandamwa na sare kwenye michezo ya ligi kuu Uingereza, hatimaye Manchester United wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Yeovil kwenye mchezo wa kombe la FA. 

Manchester United kuonyesha kuwa hawana masihara, waliweza kuwaanzisha kwenye kikosi cha kwanza nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney, Falcao na David De Gea kwenye mchezo huo.

Mchezo huo ambao ulishuhudiwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson aliyetua kwa Helikopta huku Angel Di Maria akirejea dimbani kwa mara nyingine na kufanikiwa kufunga bao la pili mnamo dakika ya 90 baada ya kiungo Ander Herrera.

Mchezo huo ambao Manchester United kwa mujibu wa bbc Sports walitawala kwa asilimiaYeovil 69, ulishuhudia vijana wa 
Yeovil wakifanya madhambi mara 13 na hii ni dalili ya matumizi ya nguvu. 

Safu ya ushambuliaji ya United ilionekana kuwa moto baada ya kupiga mashuti 18 ndani ya dakika 90 za mchezo na hii ni habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo na kocha kwani kuna dalili za timu kurejea kwenye kupata ushindi.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!