HAENDI KOKOTE- LEICESTER CITY
Na FLORENCE GR
Kwa kile kinachoonekana kutaka kuendelea kujiimarisha na kuhakikisha wanabaki ligu kuu nchini Uingereza Mabingwa watetezi wa EPL klabu ya Leicester city imekataa kumuuza mshambuliaji wake raia wa Algeria Islam Slimani kwa dau ya euro million 38 kutoka klabu ya Tianjin Quanjan ya nchini china.
Kwa taarifa za ndani kabisa inasemekana kuwa Leicester city hawako tayari kumuuza mchezaji huyo aliyesajiliwa siku ya mwisho ya usajil majira ya joto mwaka jana kwa ada iliyoweka rekodi klabuni hapo ya euro million 29 kutoka klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno huku ikifanya jitihada ya kuongeza wachezaji wengine kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Jumanne.
Timu hiyo kutoka China inajiandaa na ligi kuu chini mwao imetua kwa kasi ligi kuu nchini uingereza kutafuta wachezaji mbalimbali huku ikihusishwa pia kumtaka nyota wa West Ham United Dimitri Payet huku ikielezwa kuwa timu hiyo imeandaa mshahara wa euro 300,00 kumlipa slimani kwa wiki.
Slimani ambaye tayari ameshaifungia Leicester magoli sita katika michezo 16 aliyoichezea mpaka sasa anatarajia kujiunga na wachezaji wenzake wa timu hiyo wiki ijayo mara baada ya kushuhudiwa timu yake ya Taifa Algeria ikifungashiwa virago kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Gabon.
0 comments:
Post a Comment