Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2017
Monday, January 30, 2017

HATUMUHITAJI- WENGER









Na FLORENCE GR

Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa sasa hivi hawana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Real Madrdid mfaransa Karim Benzema hatua hiyo imekuja mara baada ya kuripotiwa kuwa Rea Madrid wamepokea ofa kutoka klabi za Arsenal na Chelsea kwenye hili dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa siku ya jumanne usiku.

Arsenal wamekuwa wakihusishwa na shambuliaji huyo raia wa ufaransa kwa miaka kadhaa sasa lakini mzee Wenger amesema kuwa hatatpeleka ofa yoyote ile ya kumtaka mchezaji huyo.

Wenger anasema kuwa 'amekuwa akihusishwa na sisi kwasababu yeye ni mfaransa na labda kwakuwa sasa hivi kumekuwa na kelele nyingi za kumtaka aondoke Madrid'.

'Hatuna hata ya kununua mshambuliaji yoyote yule kwani tunakikosi kikubwa hatuna haja na kununua wengine'.

Akiongelea kiwango kilichoonyeshwa na mchezaji Danny Welbeck ambaye ametoka majeruhi na kufanikiwa kufunga goli mbili kwenye ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Southampton katika kombe la FA.

Wenger anasema kuwa ' Welbeck amekuwa shapu lakini bado hajawa fiti alisimia zote lakini lazima tutenge muda wa kumtumia uwanjani'.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!