BIABIANY AIPIGA CHINI CHELSEA
Na FLORENCE GR
Kwa mujibu wa sky sport nchini italia inaripotiwa kuwa winga wa klabu ya soka ya Inter Milan Jonathan Biabiany amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya soka ya Chelsea ambao ni vinara wa ligi kuu Uingereza kwa sasa wakiwa na pointi 55.
Mfaransa huyo amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Inter msimu huu ambapo amefanikiwa kucheza mechi tatu tu katika mashindano yote aliyoichezea Inter.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye amechezea timu mbalimbali kama vile Chievo, Parma na Sampdoria amekataa kujiunga kwa mkopo na kutaka kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho hata kama hatapata namba kunako kikosi cha kwanza.
Biabiany ambaye mwaka 2015 alihusishwa kijiunga na klabu ya Liverpool mara baada ya timu yake ya zamani Parma kufilisika.
Chelsea wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali ya kuimarisha kikosi chao mara baada ya kuondokewa na wachezaji Oscar ambaye ametimkia ligi ya china huku Obi Mikel pia akiondoka klabuni hapo huku wakiwa na hati hati ya kuwapoteza Branislav Ivanovic na Asmir Begovic ambao wanataka kuondoka klabuni hapo.
Chelsea wanahusishwa juu ya kumuhitaji mshambuliaji wa Swansea city Fernando Llorente ,mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele pamoja na Craig Gordon ambaye ni kipa wa Celtic.
0 comments:
Post a Comment